STEVEN MAUFI AFICHUA SABABU YA KUTOHANGAIKA KUTUNGA NYIMBO SIKINDE

MCHARAZAJI magitaa wa Mlimani Park Sikinde, Steven Maufi amefichua sababu ya kutotunga wimbo wowote tangu ameanza muziki kuwa ni kuchelea kurudia visa ambavyo tayari vimeshafanyiwa kazi na wanamuziki wenzie waliotangulia.

Aidha, nguli huyo anayeweka wazi msimamo wake wa kutopenda majungu na ubinafsi, amesema kuwa wimbo bora kwake ni ule wa ‘Hali Ngumu’ alioshiriki kupiga gitaa la Rhythm akiwa na Marquis ambao amesifu kwa kusema: “Dekula Kahanga Vumbi alipiga gitaa kubwa sana la Solo.”

No comments