WIMBO 'NIMEKUZOEA' WATAKATISHA ZAIDI NYOTA YA MAROMBOSO WCB

WIMBO mpya wa msanii ambaye kwa sasa yuko chini ya lebo ya WCB, Maromoso Mshedede ‘Mbosso’ unaokwenda kwa jina la ‘Nimekuzoea’ umeonekana kukubalika za idi kwa mashabiki kiasi cha wengi kumtabilia makubwa msanii huyo.

Wimbo ‘Nimekuzoea’ ambao umeachiwa wiki hii na kutokea kuwa gumzo mjini, ni wa pili kwa msanii huyo mmoja kati ya wale wane waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band, baada ya ule alioufyatua hivi karibuni wa ‘Watakubali’.


Wakiongea na Saluti5 kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashabiki wamesema kwamba wanaamini msanii huyo atafika mbali kutokana na kuonyesha mwanzo mzuri baada ya kuvunjika kwa Yamoto Band, hasa kutokana na utulivu aliouonyesha katika tungo zake hizo mbili. 

No comments