Saluti5

Switch to desktop

SEND-OFF PARTY YA SAIDA MASHAUZI ILIVYOFANA JANA USIKU

MWIMBAJI nyota wa Mashauzi Classic Saida Ramadhan (Saida Mashauzi) jana usiku alifanyiwa sherehe za kumuaga (Send-Off  Party) ndani ya ukumbi wa Mikocheni Resort jijini Dar es Salaam.

Saida ambaye ni mdogo wake na Isha Mashauzi anatarajia kuolewa Ijumaa hiyo na bwana Ramadhan Said.

 

Sherehe hizo zilizohudhuriwa na watu wengi zilifana vilivyo na kuendelea hadi saa 1o za usiku.

Ndoa ya Saida itafungwa nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri na baadae kufuatiwa na sherehe itakayofanyika Mwika Hall Sinza siku hiyo hiyo ya Ijumaa.

Mtoto wa Isha (kushoto) na mtoto wa Thabit Abdul walikuwepo ukumbini kushuhudia sherehe ya mama yao mdogo.

Sherehe za jana zilikuwa ni "Two in One" ambapo mwanzoni ilikuwa ni Kitchen Party kwa kina mama tu kabla ya baadae kuingia kipengele cha pili cha Send Off.

 

 

Rate this item
(61 votes)

Add comment

Security code
Refresh

back to top

------- Powered by DuDumizi Solutions -------

Top Desktop version